Yohana Mbatizaji

Ni Nani Na Yu Wapi Yohana Mbatizaji?

Ielewe Biblia inasema nini kuhusu Uislam.

Imeandikwa na Paul John Mhozya.

Dar es Salaam Tanzania.

e-mail pmhozyaj@hotmail.com

Kabla hatujachunguza ni nani na yu wapi huyu Yohana Mbatizaji, tunahitaji kuchambua namna za matukio ya Kibiblia. Kwa mtazamo mwepesi matukio ya Kibiblia yapo ya aina tatu.

(1). Kuna matukio yaliyopo katika maisha ya kawaida ya wanadamu lakini yenye mwelekeo wa mafundisho katika maisha ya kiroho. Haya matukio huitwa mifano au pengine hadithi. Wakristo wote tunafahamu kuwa BWANA wetu Yesu Kristo aliishi kwa kutupatia mifano ambayo tunatakiwa kuifuata ili tuwe wana wa MUNGU. Waislamu hawaishi kukumbushana kuhusu hadithi za Mtume wao Muhammad ambazo kwao ni nguzo kubwa sana ya mafundisho katika maisha ya kila mwislamu. Si hawa tu bali hata maisha ya Mitume wengine na Manabii ni mifano kwetu.

(2). Yapo matukio ambayo yanaweza kuonekana kwa macho ya wanadamu lakini hayapo katika uweza wao. Haya tutayaita miujiza. Miujiza ni matukio yanayohusu nguvu za kiroho kutokea katika mada za kawaida zinazoonekana. Mfano katika kutoka 3:2 tunaambiwa kuwa Malaika alionekana kartika mti uliokuwa ukiwaka moto, lakini mti huo haukuungua.

(3) matukio ya juu kabisa ni ya kioroho. mara nying haya huitwa  maono na endapo yatapelekwa kwa wanadamu ili wayajulishwe huitwa funuo. Labda kwa nadra sana maono au funuo huwatokea watu wa kawaida. mara nyingi matukio haya huwatokea Mitume na Manabii wa MUNGU. katika matukio haya BWAN hunena au:

(i) Moja kwa moja kwa vinywa vya manabii hawa.

(ii) Huwafunulia manabii hawa na kuwatuma wakawaambie( wawatafsirie) wnadamu yale waliyoyaona na kuelekezwa.

Ni kunena huku kwa BWANA kwa Watumwa wake kuhusu maisha yao yajayo hasa hasa ndiyo wengi wetu tunaita funuo.  Yote haya ambayo tunayakuta katika mandiko matakatifu mlengwa ni ulimwengu na hasa mwanadamu ajue neno la BWANA MUNGU wetu kwa waja wake.

Pamoja na kuwepo mitazamo na tafsiri mbali mbali za matukio na funuo za kibiblia, jambo moja ambalo huwezi kulificha ni kuwa matukio yote huishia kuwa "KWELI" katika maisha ya kawaida ya wanadamu. Funuo zilzopita zikifuatiliwa kwa makini utakuta matukio yake na miujiza yake vyote vilishatokea. BWANA ndiye Mweza na ukifikiria jinsi walivyowaza wanadamu wakati alipowaambia kuwa; 

 

utakutana na hali ile ile ya kutatanika kutafuta tafsiri za ajabu ajabu kama ambavyo viongozi wetu wa dini wa sasa wanajaribu kutafuta tafsiri ya maandiko ambayo wanadhani yamefumbwa. Lakini BWANA hakufumbia watu kwani ni hivyo hivyo ndivyo lilivyokuwa. Ni hivyo hivyo kuwa tusijaribu kutafuta mafumbo katika Biblia bali tutafute maisha yetu ya baadaye. Kama matukio yalishapita basi tutafute tu kama ni ya kawaida au ni miujiza. Hivyo tunahitaji tu kuwa wangalifu kutafuta matukio yanayolingana na funuo tunazozikuta badala ya kwenda tunatafuta "siri zilizofichika" katika mandiko matakatifu. MUNGU hunena juu yetu na matukio hayo hutokea kwetu wenyewe. Tatizo ni lini na wapi, basi!!! Tuchukue mfano wa Mtume Ibrahim alivyofunuliwa na BWANA kuhusu uzao wake:

 ß

ß

ß

ß

ß

Amini usiamini Ufunuo huu haukuwa na fumbo kuhusu haya. Hivyo hivyo unashauriwa kutokwenda ukitafuta mafumbo katika Biblia, tafuta matukio ya kawaida au sana sana miujiza.

Kufunuliwa kwa Yohana Mbatizaji

Kabla ya kuzaliwa kwake Yohana Mbatizaji alifunuliwa na BWANA MUNGU wetu kwa Ulimwengu wazi zaidi kupitia Malaki. Habari zinazoonekana kufunuliwa na Malaki zinakuja kuthibitika baadaye wakati Yohana Mbatizaji alipozaliwa kama ifuatavyo:

ß

Pia katika Malaki na baadaye katika Luka tunasoma yafuatayo:

ß

 

Yohana Mbatizaji na Eliya

Katika Biblia kuna ushuhuda wa kutosha kuwa Yohana Mbatizaji ndiye Eliya, isipokuwa tu katika jina na katika wakati. Kwanza kabisa tunakumbuka BWANA aliahidi kumleta Eliya tena wakati wa Malaki (Malaki 4:5-6). Kuja huku kulishuhudiwa na Zakaria katika ujumbe wa Malaika wakati wa kuzaliwa Yohana (Luka 1:17). Pamoja na shuhuda hizi kuna ushuhuda uliotoka kwake BWANA wetu Yesu Kristo hata baada ya Yohana Mbatizaji kutoka katika dunia kama ambavyo imeandikwa:

 Hatma ya Ulimwengu

Kurudi kwa Yohana Mbatizaji na kuzaliwa kwa Imani ya Uislamu vyote tunavikuta katika Ufunuo wa Yohana Mtume. Kama kawaida ya funuo nyingi maono katika Ufunuo huu  ni ya kiroho na siyo ya namna ya kuonekana moja kwa moja kwa macho ya kibinadamu

lakini wote wanaoonekana katika roho wana sifa ambazo katika maisha yao ya kidunia hazifichiki. Kwa mfano BWANA wetu Yesu Kristo anaonekana kama alivyofahamika kuwa alifananishwa na Mwana-Kondoo

Vivyo hivyo tunafahamu kuwa Yohana Mbatizaji ndiye Nabii wa Ufunuo wetu huu ambaye alikatwa kichwa wakati akiwa gerezani.

Na tuanze kwanza kuangalia hatma ya Ulimwengu ili kuunganisha shuhuda za kweli ambazo baadaye zitatuweka mahala pazuri pa kuelewa vizuri zaidi ukweli kuhusu nabii Yohana Mbatizaji. Hapo juu nimesema " Ufunuo wetu huu" kwa sababu kila ufunuo unahusu watu. Isaya, pamja na kutufunulia ujio wa BWANA wetu YESU KRISTO, mara nyingi zaidi  alitabiria wana wa Israeli kulingana na matendo yao ya wakati huo. Sana sana tunasoma funuo hizi ili kujifunza mambo yaliyowafika wanadamu wakati huo na kujua ni matendo gani walitenda ya kumpendeza Mungu na yepi yaliyowaletea hasira za MUNGU. Katika hayo tunatakiwa kwenda kujifunza tu na siyo kutafuta maisha yetu. Kuna ushuhuda wa kutosha kuwa Ufunuo wa ulimwengu wa sasa ni wa Yohana Mtume ambao una matukio mengine ambayo tayari yalishatokea.

Matukio yenye hatma ya ulimwengu yaliwekwa katika uweza wa BWANA wetu Yesu Kristo mara alipopewa kitabu kilichotiwa muhuri:

ß

ß

 

Ni kuanzia hapa kuwa tunaona shuhuda mbali mbali ambazo zinaweza kudhihirisha matukio halisi yaliyokwishatukia katika ulimwengu huu.

Muhuri wa kwanza

Hapa tunao ushuhuda wa kuenea dunia nzima ukoloni wa Wazungu na hasa hasa "Falme" ya Kiingereza. Misemo ya "Jua halitui katika Himaya ya Waingereza" ni jambo la vyema kulikumbuka. 

Muhuri ya pili

Farasi mwekundu huyu kazi yake ilikwishatekelezwa katika dunia wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia. Historia inasema hata kuwa wazungu walikuwa wakigombania kulinda makoloni yao. Watukutu kama Hitler hawakujulikana hata waliibuka vipi na kwenda wapi baadaye.

Muhuri ya tatu

Baada ya kufunguliwa muhuri ya tatu

Katika kufunguliwa kwa muhuri hii tunaukuta Umoja wa mataifa ikiunganisha mataifa yote katika amani na biashara. Tunakuta nchi za Kiafrika na hata Tanzania zikitafuta uhuru wake kutoka kwa Wakoloni kupitia umoja wa Mataifa.

Haya ni matukio makubwa ya kiulimwengu (global), lakini yapo pia matukio ya kikanda na kimkoa ambayo tunahitaji kukutana na wale walioyashuhudia ili kuupata ukweli wake.

Kurudi kwa Yohana Mbatizaji na Kuja kwa Uislamu

Matukio yaliyo na tafsiri ya kurudi kwa Yohana Mbatizaji yanaanzia pale ambapo imani mpya inateremshwa kutoka kwa MUNGU. Kwanza tukumbuke kuwa katika maandiko matakatifu ishara yeyote inayotaja mwali, bibi arusi au mwanamke mara zote ni imani, au kwa Wakristo ni kanisa. Bwana Arusi daima ni BWANA MUNGU wetu au MWANAE wa pekee BWANA wetu YESU KRISTO, na waalikwa katika arusi au katika makusanyiko ni waumini. Katika Ufunuo wa Yohana Mtume imani yenye kuwa na ishara ya nyota na mwezi, na ambazo ndiyo alama zinazotumika katika Imani ya Waislamu, ilionekana.

Wakati imani hii ikishushwa kwa watu BWANA wetu YESU KRISTO alikuwa akiungana (katka Roho) na BABA na kuwa MUNGU mmoja. Hapa tunaona kuwa BWANA YESU KRISTO akitoka katika sifa ya Mwana-Kondoo aliyechinjwa na kwenda katika Sifa ya MUNGU ambaye alijulishwa kwetu kuwa YEYE ni ALFA NA OMEGA au MWANZO NA MWISHO.

Bahati mbaya kuwa wakati imani hii inateremshwa kwa watu kulikuwa na hasira kuu mbinguni. Hasira ya MUNGU juu ya damu ya nabii wake Yohana Mbatizaji ilikuwa kuu kasi cha kufyeka waliokuwa katika maisha kama ambavyo imeandikwa

Tutatambua kuwa hatari ya joka hili ilitokana na kumwagika kwa damu ya Yohana Mbatizaji na hii ndiyo sababu  ni yeye Yohana Mbatizaji ( huku akiwa na alama zile zile zilizopewa joka, yaani vichwa saba na pembe kumi) ndiye anayekuja kupewa mamlaka ya kisasi cha hasira hizi juu ya wanadamu kama ambavyo imeandikwa:

ß

Wakristo wote tunajua kuwa tunayo ahadi ya kurudi tena kwa BWANA wetu Yesu Kristo. Na ili lipate kutimia neno kuwa Eliya ndiye atakayetangulia kuja kwake BWANA katika siku zile za mwisho,

ß

 

 ili watu wapate kuwekwa tayari kwa BWANA, Yohana Mbatizaji, ambaye tulijulishwa kuwa ndiye Eliya ni sharti atangulie na hivyo alipewa heshima yake ya unabii kwa wanadamu ili yapate kutimia yale yaliyokwishanenwa.Ujio wake huo ulioonekana katika ishara ya mnyama wa mwisho ambaye ndiyo alikabidhiwa mamlaka ya joka na ya mnyama wa kwanza, kama ambavyo iliandikwa:

Hata hivyo ujio wake huu haukumnyang'anya mamlaka yake kutekeleza adhabu ya MUNGU juu ya watu hivyo alipewa mamlaka yote yaliyotoka kwa joka na kwa mnyama wa kwanza. Pamoja na kujulishwa kuwa mnyama huyu alikuwa na sifa za kutokea juu ya nchi, tunafahamishwa pia kuwa mnyama huyu wa mwisho ni mwanadamu na ambaye amefumbiwa namba 666.

 

Kwanza hapa tunatakiwa kufahamu kuwa mwenye hesabu pekee ambaye anajulikana kwa wakristo ni BWANA wetu YESU KRISTO. Miaka katika dunia inakwenda kwa HESABU yake ya Anno Domino (AD au Baada ya Kristo). Hapa sasa ni sharti tuingie katika mahesabu tena kidogo ili kuweza kumpata mzaliwa mwingine mwenye sifa ya kuwa na HESABU yake ambayo ipo kati ya wanadamu. Mtu mwenye sifa ya Utume au Unabii aliyekuja baada ya kuanza HESABU ya miaka ya BWANA wetu YESU KRISTO si mwingine bali ni Mtume Muhammad wa imani ya Waislamu ambaye miaka yake ina hesabu ya Anno Hijra (AH). Historia ya Waislamu inasema kuwa Mtume Muhammad alizaliwa mwaka 570 AD ambayo kwa maneno mengine ni karne ya sita. Mtume Muhammad alitoka duniani mwaka 634 AD. Kwa hesabu hii hatujampata, kwanza siyo hesabu yake, halafu katika imani yake yeye YESU KRISTO si MUNGU bali ni Nabii Issa mwana wa Mariam. Moja kwa moja hapa tunaanza kumpata mwenye sifa ya MPINGA KRISTO.

Tukienda sasa katika hesabu yake yeye tunakuta mwaka wa AD mmoja una siku 11 zaidi ya mwaka wa AH, hivyo ili kuipata hesabu ya Mtume Muhammad tunatakiwa kuhesabu miaka katika namba za AH na siyo AD. Kuna fomula mbali mbali za kubadilisha miaka kutoka AD kwenda AH na moja rahisi ambayo nitaitumia hapa ni AH=AD + AD/32, kwa hiyo katika vipimo vya AH Muhamaad alizaliwa mwaka 588 baada ya Kristo, ambayo ni karne ya sita. Mtume Muhammad alitoka duniani mwaka 654 baada ya Kristo. Kumbuka tu kuwa hapa tumehesabu urefu wa miaka kwa vipimo vya mwaka wa AH ambao ni mfupi kwa siku 11 na unakwenda na mzunguko wa mwezi. Hivyo katika hesabu hii Muhammad aliishi jumla ya miaka 66. Na hapa tayari tunapata hesabu ya mnyama wa pili ambayo ni "karne ya sita ya kuzaliwa, na miaka sitini na sita ya kuishi kwa Mtume Muhammad". Sifa ya mpinga Kristo tayari tumekwisha kuitaja, na sifa ya Uislamu kutumia alama ya nyota na mwezi pia tumeitaja.

Imani kuwa nyikani

Tunakumbuka kuwepo kwa imani ya Ufunuo wa Yohana iliyoshushwa duniani wakati kukiwa na hasira kuu ya Mungu kwa kuuwawa kwa Nabii wake Yohana. Tunafahamishwa kuwa stahiki ya wanadamu kupelekewa imani hii ya upendo kulikuwa mashakani kwani hasira za Mungu ziligubika kustahiki huko

 

Kitendo cha Uislamu kutomjua BWANA wetu YESU KRISTO ni kitendo cha kutomjua mwalikaji wao katika imani. Hivyo imani yao haiko nyumbani kwa BWANA bali ipo porini au nyikani. Badala yake MUNGU amempa fadhila zake Yohana Mbatizaji ambaye ni "Mwitwa katika Upendo" ili waalikwa katika imani hii  wamtaje kama "Msifiwa" ambayo ndiyo maana ya jina Muhammad. Na Waislamu kweli humsifu Mtume wao kila wanapotaja jina la MUNGU. Lakini wapo waliopindukia mipaka na kuingia katika ufisadi wa kidini kwani wao hata kwa MUNGU hawaendi bali wanafaidika tu na "majini'

ambazo ndiyo nguvu zilizopelekwa na fadhila ya Yohana Mbatizaji ili watakaojua jina la Mungu katika sifa wapate kuishi bila woga.

Hata hivyo kuna mwisho wa kuwepo nyikani kwa imani hii na kwamba watakuja waumini wa kweli wanaolijua jina la MWANA wa MUNGU, kama ambvyo imeandikwa

 Je aliyempinga Kristo alipewa siku ngapi kuendesha uasi wake?

John alibarikiwa nguvu nyingi juu ya wanadamu ambao wakati huo ndiyo walipelekewa laana kwa sababu ya kumkata kichwa

Hata hivyo uweza huo ulikuwa ni kwa muda mfupi tu kama ilivyoandikwa

Uweza huu kibinadamu tunaufahamu kama uweza wa kishetani au uasi. Siyo Yohana Mbatizaji aliyeleta uasi huo bali ni dhambi ya damu yake ndiyo iliyoleta uasi huo kwani kwayo Mungu alileta hasira yake na laana katika dunia na wote waliolaaniwa wapate kulipizwa. Hivyo nabii Yoahana aliachiwa atie uasi katika ulimwengu ili wote waliolaaniwa wamuasi Mungu wapate kuadhibiwa.

NB. Inafaa ikumbukwe tu kuwa MUNGU ndiye BWANA, hakuna anayeweza kumuasi bali matendo ya wanadamu ndiyo yanaweza kusababisha MUNGU akawapatiliza kutokana na matendo yao.

JE Uislamu ni Upotofu wa kuleta kuangamia?

Tujifunze kuona Waislamu walivyo na muelekeo wa kuvuka hata udugu wa damu katika imani yao. Wengine wko radhi hata kupigana kwa sababu zisizojulikana kwao ili muradi tu wamesikia Muislamu mwenzao amesema ( hata kwa uongo) kuwa anaonewa. Hawa ndiyo walioandikiwa hivi

neno lililokuja rudiwa tene wakati wa kuzaliwa Yohana Mbatizaji ambapo Malaika  Gabriel alimwambia Zacharia

Mengi sana yaliyotajwa katika ufunuo wa Yohana yanatokea katika imani ya Uislam. Utawaona Waislam wakiungurumisha "kaswida" za kumsifu mtume Muhammad kama ilivyoandikwa

Hapa swala la "mnyama" siyo la msingi kwani katika maisha ya BWANA maumbile ni uwakilishi takatifu, hauna maana ya sifa za upungufu au ushetani tunaoufikiria duniani. Hata viumbe wenye uhai waliokuwa wakishangilia kufunguliwa mihuri ya hatma ya dunia walikuwa na maumbile mbalimbali. Mmoja alikuwa kama Simba, mwingine kama Ng'ombe, wa tatu kama Tai na wa nne ndiye alikuwa kama Mwanadamu.

Tatizo hapa kwetu ni tafsiri ya kumsujudia mnyama kwani hakuna imani inayomsujudia kiumbe. Ni pale tu penye laana ndipo Mungu huwaacha wanadamu kwa kuwa wanakuwa "wamechafuka" na kuwa chukizo kwake. Hivyo kwa MUNGU " mnyama" huyu alistahili SIFA tu na siyo kusujudiwa. Na SIFA ndiyo aliyopewa Yohana Mbatizaji na kuletwa tena ulimwenguni akiwa na jina la "Msifiwa" au Muhammad.

Waislam wamepungukiwa sifa moja tu nayo ni kuwa waalikwa katika karamu za BWANA wa Karamu Mwana wa MUNGU BWANA wetu YESU KRISTO ambaye ndiye alizaliwa MBINGUNI katika imani hii mpya kwani ilitokea wakati BWANA wetu YESU KRISTO ametwaa mamlaka hatma ya ulimwengu

Waislam hawaendi na BWANA wa Karamu hivyo makusanyiko yao hayako nyumbani kwa BWANA bali Nyikani.

Je kumwekea tayari watu waliotengenezwa kunaonekena pia? Tukumbuke hata Mitume wa zama za BWANA wetu YESU KRISTO walisali sala tano

Hata Wamissionari, Mapadri na Watawa sala hizi wanafahamu kuwa ni wajibu, lakini tu kuna upotofu ulioletwa na wapotoshaji waliokuwa wanatafuta nafuu katika maisha kwa kuona ugumu wa utekelezaji wa amri hii katika mazingira ya watu wa kawaida. Waislamu wenye imani ya kweli wanajua kuwa sala hizi ni nguzo moja wapo ya imani yao. Imani na Ibada haviwezi kutenganishwa, hivyo utii huu unawapeleka waislamu katika maisha ya kumtukuza MUNGU zaidi kuliko katika maisha ya dhambi.

Kuna kivutio katika Uislam, nalo ni (hapa tuite kwa lugha rahisi tu) JINI. Mwislamu, kwa kupitia aya za Mtume tu anaweza kupata nguvu za ajabu ambazo vinginevyo hazipo.

 Nguvu hizi mara nyingi zimetumika kuleta madhara hivyo hujulikana ni nguvu za shetani au Majini. Mwisho wa Uislamu utaletwa na maangamizi ya kutaka kutumia  nguvu hizi kwa maonevu badala ya kujihami wakati wa hatari. Lakini hii inasababishwa na kazi ya roho mwenyewe aliyetumwa kufanya miujiza juu ya nchi kwani imenenwa

Inaaminika kuwa uonevu aliotendewa Yohana Mbatizaji ndiyo chimbuko la Nguvu hizi za kinga ili waumini wa dini iliyopelekewa mtume duniani wasionewe tena.

Lakini badala ya kinga, sasa ni Biashara, uuaji na uchafuko mwingine mwingi usiokuwa na maana tena. Waislam wengine wamo katika imani si kwa kuwa wanamtukuza MUNGU bali kwa sababu kuna Biashara, "uwezo" na mambo mengine ya kiulimwengu yanayoweza kuletwa na nguvu za majini. Na hapo ndipo palipo na nyika hasa na maangamizi yanayoweza kutokana na dini ya Uislam.

Je mwisho wa Uislam umetabiriwa pia?

Inawezekana kuwa hili lipo pia. Uislam wa mwisho unatarajiwa utaondoka huko nyikani kwa kuwa umepelekwa huko kwa muda tu kama ilivyonenwa

na kushinda nguvu za laana ambazo pia zimepewa muda maalumu wa kufanya kazi yake kama ilivyonenwa

Baada ya Uislam huu wa mwisho watatokea wanaomjua  BWANA wa karamu ambaye ni KRISTO mwana wa MUNGU

Baada ya ukweli huu yatustahili kujua endapo mapigo saba ya mwisho ya gadhabu ya MUNGU yamekwitimia? Vinginevyo yaja na yamekaribia kwani katika mapigo haya  Uislamu wa zamani ( usiomjua KRISTO) utaangamizwa

Pia tunasoma kuwa nguvu uovu na laana ya MUNGU juu ya wanadamu vitatoweka na wale watakaokuwa wakiishi katika imani hiyo watahangaika na kusononeka;

yawezekana kabisa kuwa kitasa cha sita cha gadhabu ya MUNGUmatokeo yake wote tumeyashuhudia hivi karibuni kwa Marekani kuivamia na kuikalia Irak, kwani yamenenwa hivi:

Ifahamike kuwa kukauka mto Frati siyo kuishiwa maji ( kama ambavyo maji ya mito yote kugeuka damu,siyo kuwa na maji yenye rangi nyekundu yenyewe kama damu). Pia mawio ya jua  siyo lazima yalingane na mistari iliyochorwa na wanadamu wa sasa (Wazungu) kugawa ulimwengu katika Magharibi na Mashariki. Yawezekana kabisa katika Ufunuo ( hata kigeografia) Marekeni ipo mawio ya jua ya Irak.